Breaking

TANGAZO...|| PAKUA/ DOWNLOAD APP YA "TWAPLUS APP" USOME HABARI ZOTE HATA USIPOKUWA NA MB... BOFYA HAPA CHINI

Friday, 20 April 2018

April 20, 2018

MICHEZONI LEO


inazo endelea kubamba ni raia wa Togo anae kipiga huko Ethiopia ktk club ya walloyta dicha FC #arafat djako kuhitajika jangwani

Kiukweli ni mzuri anauwezo wa kumiliki na kukimbia na mpira hata finishing yupo OK.

Swali je scout ya yanga imejiridhisha  na afya ya huyo mchezaji

 Ameonekana 2 game kucheza vizuri na zinatosha kujiridhisha lkn afya ndio kila kitu

Musiingie chaka yanga mukaja ongeza majeruhi jangwani.

 Kupotea njia ndio kujua njia
April 20, 2018

MPEKESA TRANSPORT IMEFIKA IFAKARA


E
WEWE NI MWENYEJE WA IFAKARA?

NA UNAPATA SHIDA KIPINDI HIKI CHA MASIKA?

KWA USAFIRI WA KUTUMA KIFURUSHI NA HATA MWENYEWE NDANI YA IFAKARA BASI MPEKESA TRANSPORT YUPO KWA AJIRI YAKO
KWA USAFIRI WA NDANI HADI KWAKO TUTAKUFIKIA

VYOTE HIVI VITAANZA JUMATATU

KWA MAWASILIANO
       0717067052
       0788689940
UKIPIGA SEMA MPEKESA NAHITAJI BAJAJI AU BODA BODA NA ENEO ULILOPO TUTAKUFIKIA
April 20, 2018

HATUNAYE YENAA


REAKING: Taarifa zilizotufikia muda huu ni kwamba Video Vixen maarufu Agnes Gerald 'Masogange' amefariki dunia katika Hospital ya Mama Ngoma Mwenge. Imethibitishwa na Wakili wake.

Rest In Peace Agnes Gerald "Masogange"
April 20, 2018

ASSISTANT LECTURER (MARINE OR MECHANICAL ENGINEERING ) – RE ADVERTISED - 1 POST

ASSISTANT LECTURER (MARINE OR MECHANICAL ENGINEERING ) – RE ADVERTISED - 1 POST
Employer: National Institute of Transport (NIT)
Date Published: 2018-03-28
Application Deadline: 2018-04-11
SANITARY HAND KIBAHA EDUCATION CENTRE (KEC)


JOB SUMMARY:
N/A
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
(i)    Teaches up Bachelor Degree (NTA level 8 or equivalent) including assessment, prepare learning resources for tutorial exercises,
(ii)    Conducts research and seminars,
(iii)    Carryout consultancy and community services.
(iv)    Supervise students’ projects,
(v)    Prepare teaching manual
(vi)    Performs any other duties assigned by supervisor

QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Master's degree, with a GPA of not less than 3.5 at Bachelor’s degree and 3.8 at Master’s degree level and for unclassified degrees, overall average of not less than B grade from a recognized institution.
REMUNERATION: Salary Scale Government salary scale PHTS 2.1
Login to Apply

Thursday, 19 April 2018

April 19, 2018

MAGUFULI KIBOKO KWA HILO


TUAMBIZANE UKWELI*

Leo hii baadhi ya Watu wanaona wamepata cha kuongea kuhusu pesa Tsh. Trillion 1.5 eti wanadai zimeibwa na Rais Magufuli, dhambi ya hali ya juu.

Trilioni 1.5 si kitu mbele ya Rais Magufuli endapo angeamua kutumia vibaya kofia yake ya Urais.

Kwa kuonyesha hata tamaa ya kuiba pesa wala kuchota rasilimali ya Taifa ndio maana;-

1. Kazuia mchanga wa madini kusafirishwa nje kienyeji.

2. Kazuia usafirishwaji wa Wanyama hai nje ya nchi.

3. Kawabana wachimbaji wa madini wa mataifa ya nje ili nchi inufaike

4. Kajenga ukuta mkubwa wa kuzunguka Mererani mahali ambapo kunachimbwa madini ya Tanzanite ili kuzuia utoroshwaji wa madini yetu.

5. Amezuia vilivyo upotevu wowote ule pale Bandarini kwa kuhakikisha flow meter ya kupima mafuta inafanya kazi, kuhakikisha mfumo wa ukaguzi wa utoaji wa vitu unajulikana ili mapato yakusanywe vyema.

6. Amezuia posho na semina za ovyo ovyo ndio maana sasa hivi hakuna tena uozo huo uliokuwa unawanufaisha wachache.

7. Amezuia safari za nje zisizo na tija, ndio maana hata yeye hasafiri safiri ovyo ovyo nje ya nchi.

8. Amefuta pesa za posho na vitafunwa pale Ikulu na kwenye maofisi yote ya umma ya Serikali na pesa kuzielekeza kwenye fungu la maendeleo.

9. Amewatimua wenye vyeti vyeki na Watumishi hewa Serikalini. Hii imesaidia kuzuia matumizi mabaya kodi za Watanzania.

10. Anahakikisha makusanyo ya kodi za ndani yanaimarika zaidi kwa kudhibiti kila kona aina zote za upotevu wa mapato. Leo hii malipo hayafanywi kwa risiti za kuandikwa kwa mkono bali hufanyika benki ama kwa kutumia mashine za EFD's.

Wanaosema Rais Magufuli ameiba hawajui nguvu na madaraka aliyonayo Rais. Endapo angetaka kuwa mpigaji asingeyafanya hayo yote wala Serikali yake isingewapandisha kizimbani Mafisadi papa na Wahujumu uchumi.

*Historia Kujirudia?*

Ni kawaida ya Binadamu kutokuwa na shukrani. Historia hapa nchini inaonyesha ni kawaida kwa Marais wanapokuwa madarakani kudhihakiwa, kutukanwa na kubebeshwa kila aina ya lawama. Lakini hukumbukwa sana pindi wanapotoka madarakani.

Tuweke kumbukumbu zetu sawa. Mwalimu Julius Nyerere wakati akiwa madarakani alimwagiwa lawama na tuhuma lukuki kwani wapo waliosema Mwalimu haambiliki na wengine wakadai anaendesha nchi kwa “remote” akiwa Butiama (kijijini kwao). Lakini mara baada ya kung’atuka kwa hiari Urais ndipo sifa za kinafki zilianza kummiminikia huku tukianza kumuita “Baba wa Taifa”. Mara baada umauti kumkuta ndipo unafki ulizidi kwake na leo hii kila kitu kibaya kinachotokea tunasema laiti Mwalimu Nyerere angekuwepo haya yote yasingetokea. Lakini angali hai ama madarakani hatukuyatambua haya zaidi ya kuuendekekeza unafki.

Ama Alhaji Hassan Mwinyi wakati akiwa Rais wa awamu ya pili walimwita mbinafsi, muuzaji nchi kutokana na ubinafsishaji lakini leo hii ni mstaafu wanaanza kummwagia sifa teletele  na hata kumwita “Mzee wetu” huku wakijivunia kuchota hekima na busara kutoka kwake lakini angali madarakani hatukuliona hilo. Huu ni unafki mtupu.

Pia  Benjamini Mkapa alidhihakiwa kweli kweli wakati wa uongozi wake hadi kufikia hatua ya kumwita ‘ukapa’ badala ya Mkapa kutoka katika neno la ‘ukata’. Lakini leo hii kila anapokatiza ni shangwe, makofi, vifijo, na vigelegele na tukisema afadhali ya Mkapa kuliko wote na wengineo tumewaona wakimpa hata tuzo ya heshima. Jamani! Kama huu si unafki, basi tuuiteje?

Hata Dk. Jakaya Kikwete (JK) alipokuwa madarakani walimuita majina mengi ya hovyo hovyo. Wapo waliomuita “Mzee wa kutabasamu”, Serikali yake ni dhaifa na legelege! Lakini hekima na busara kubwa aliyojaaliwa Dk. Kikwete hakuweza kuwajibu lolote waliokuwa wakimkejeli na badala yake aliwaambia mtanikumbuka.

Kikwete alisema: “Mtaumbuka baada ya 2015”. Dk. Kikwete aliwaambia wanaombeza sasa wataona aibu baada ya kumaliza kipindi chake. Naam! Ni kweli Watu waliokuwa wakimbeza wameanza kuumbuka na kunza kupayuka hadharani kuwa wana mkumbuka.

Wale waliokuwa wakidai JK ni legelege na dhaifu wanataka Rais mkali ndio hao hao leo hii wanasema Rais Magufuli ni dikteta; Wale waliokuwa wanasema JK hawezi kuchukua maamuzi magumu ya kutimua wanaoharibu, ndio hao hao leo hii wanaosema kuwatumbua “kuwafukuza”  wanaoharibu ni kinyume na haki za binadamu; Mara JK hakamati mafisadi Papa ama hawakamati wauzaji madawa ya kulevya, leo hii wameanza kukamatwa wanaanza kuwatetea kwa kusema si vyema kuwataja watu majina, mara si vyema kuwakamata waliolitumikia Taifa letu!

Huu ni unafki mkubwa unaoliangamiza Taifa kwa sisi Watanzania kutokuwa wakweli na kuamua kujivisha sura ya undumila kuwili.

*Rais Magufuli angeamua kuwa Mpigaji asingefanya makubwa yote haya ...*

Rais Magufuli ndani ya kipindi kifupi ameweza kufanya mambo makubwa sana yanayogharimu mabilioni kama sio matrilioni.

1. Amenunua ndege mpya sita

2. Ameanzisha ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha standard gauge inayotumia umeme.

3. Amejenga Barabara za juu (flyovers) pale Tazara na Ubungo

4. Anatoa Elimu Bure kuanzia shule ya msingi mpaka Sekondari ambapo kwa kilo mwezi hutumia Tsh. Bilioni 24

5. Ameboresha sekta ya Afya kwa kiwango kikubwa. Leo hii Luna hospital na Wataalamu bingwa wanaofanya operesheni kubwa hapa nchini ambazo awali nilikuwa zinapatikana nje ya nchi, Leo hii upatikanaji wa madawa ni wa kuridhisha mahospitalini ambapo umefikia asilimia 89.

6. Amejenga mabweni ya Wanafunzi chuo kikuu na ya Polisi.

7. Ndani ya muda mfupi kero ya ukosefu wa madawati iliyodumu kwa muda mrefu imebaki historia shuleni.

8. Serikali yake inajitahidi kulipa madeni ikiwemo kulipa deni la Taifa na kupunguza madeni ya ndani kwa Wataalamu na Watumishi wa umma.

9. Amehakikisha fumbo gumu la Serikali kuhamia Dodoma linakwisha kwa Wizara mpaka Waziri Mkuu kahamia Dodoma.

10. Ameanzisha miradi mikubwa ya kuzalisha umeme nchini na kuhakikisha umeme unaenda mpaka vijijini kupitia mradi wa umeme vijijini wa REA.

*Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni*

Rais Magufuli ni Mzalendo, Shujaa, Mpenda haki, Mtetezi wa Wanyonge na Mjenzi imara wa Taifa letu wa kipindi chote.

*Na Emmanuel J. Shilatu*
April 19, 2018

KING MSWATI AZUA JAMBO TENA


King Mswati III atangaza jina jipya la nchi yake
Mfalme wa Swaziland, King Mswati III ametangaza kubadili jina la nchi hiyo na sasa itaitwa Kingdom of eSwatini ikimaanisha Ufalme wa Waswati.
Mfalme huyo ametangaza mabadiliko ya jina hilo rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Swazi.
Sherehe hizo pia zimeadhimisha miaka 50 ya mtawala huyo ya kuzaliwa. Taifa hilo lililoko kusini mwa Afrika ni taifa lililokwenye utawala kamili wa Kifalme.
Mfalme huyo anayejulikana kwa jina la Ngwenyama au "Simba", anajulikana kwa kuwa na wake wengi na uvaaji wake wa kitamaduni.
Swaziland pia ni nchi mwanachama wa Jumuia ya Madola.
Hata hivyo kwa mujibu wa BBC mara baada ya kutangazwa mabadiliko ya jina hilo, inasemekana kuamsha hasira miongoni mwa wananchi nchini humo na ambao wanaamini kuwa Mfalme huyo alipaswa kuangalia zaidi masuala ya uchumi usiokuwa wa Taifa hilo.