Breaking

TANGAZO...|| PAKUA/ DOWNLOAD APP YA "TWAPLUS APP" USOME HABARI ZOTE HATA USIPOKUWA NA MB... BOFYA HAPA CHINI

Thursday, 19 April 2018

KING MSWATI AZUA JAMBO TENA


King Mswati III atangaza jina jipya la nchi yake
Mfalme wa Swaziland, King Mswati III ametangaza kubadili jina la nchi hiyo na sasa itaitwa Kingdom of eSwatini ikimaanisha Ufalme wa Waswati.
Mfalme huyo ametangaza mabadiliko ya jina hilo rasmi katika maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Swazi.
Sherehe hizo pia zimeadhimisha miaka 50 ya mtawala huyo ya kuzaliwa. Taifa hilo lililoko kusini mwa Afrika ni taifa lililokwenye utawala kamili wa Kifalme.
Mfalme huyo anayejulikana kwa jina la Ngwenyama au "Simba", anajulikana kwa kuwa na wake wengi na uvaaji wake wa kitamaduni.
Swaziland pia ni nchi mwanachama wa Jumuia ya Madola.
Hata hivyo kwa mujibu wa BBC mara baada ya kutangazwa mabadiliko ya jina hilo, inasemekana kuamsha hasira miongoni mwa wananchi nchini humo na ambao wanaamini kuwa Mfalme huyo alipaswa kuangalia zaidi masuala ya uchumi usiokuwa wa Taifa hilo.

No comments:

Post a Comment