Breaking

TANGAZO...|| PAKUA/ DOWNLOAD APP YA "TWAPLUS APP" USOME HABARI ZOTE HATA USIPOKUWA NA MB... BOFYA HAPA CHINI

Monday, 12 March 2018

Rais Magufuli asisitiza kuilinda amani ya nchi


Rais Magufuli asisitiza kuilinda amani ya nchi
Rais John Magufuli amesisitiza kuwa atailinda kwa nguvu zake zote amani ya Tanzania iliyoasisiwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere kwani amani ndiyo chachu ya maendeleo ya taifa.
Pia amewaomba viongozi wote katika nyanja mbalimbali ikiwemo dini, siasa na wananchi wote kushiriki katika utunzaji wa amani ya nchi.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi katika uzinduzi wa Barabara ya Uyovu-Bwanga iliyoko wilayani Bukombe mkoani Geita yenye urefu wa kilomita 45, iliyogharimu shilingi bilioni 47, fedha zote zikidaiwa kuwa ni za ndani.
Amesema “Pasingekuwa na amani, hii barabara isingetengenezwa, hiyo hela ingetumika kwenda kutengeneza amani ya nguvu”.
Aidha, Rais Magufuli amesema ujenzi wa barabara hiyo kwa fedha za ndani, ni uthibitisho kuwa Watanzania wana uwezo wa kujiletea wenyewe maendeleo bila kutegemea misaada kutoka nje.
“Watanzania tuna uwezo lakini wapo watu walikuwa wanawajengea dhana kwamba Tanzania sisi hatuwezi, akitokea mtu akasema tunaweza, anageuka kuwa adui. Watanzania hawapaswi kuwa masikini, hawapaswi kuwa ombaomba, Tanzania ni tajiri,” alisema Rais Magufuli.

No comments:

Post a Comment