Breaking

TANGAZO...|| PAKUA/ DOWNLOAD APP YA "TWAPLUS APP" USOME HABARI ZOTE HATA USIPOKUWA NA MB... BOFYA HAPA CHINI

Sunday, 11 March 2018

Bunge la China launga mkono Xi Jinping kusalia madarakani


Bunge la China launga mkono Xi Jinping kusalia madarakani "maisha yake yote"
Bunge la China limepiga kura ya kuridhia mabadiliko ya katiba ambayo yameruhusu kuondolewa ukomo wa muda wa uongozi wa rais.
China ambayo ilianzisha utaratibu mihula miwili kwa rais wa nchi hiyo kwenye miaka ya 1990 imeamua kuondoa ukomo huo na sasa rais wa nchi hiyo, Xi Jinping huenda akasalia madarakani kwa muda wote wa uhai wake.
Wabunge 2,964 ndio walioshiriki zoezi la upigaji kura kwenye muswada huo na kati ya kura hizo ni wabunge wawili tu ndio waliopinga pendekezo hilo huku wabunge watatu wakikataa kuonyesha msimamo wao.
Rais Xi Jinping alitarajiwa kumaliza muda wake wa urais mwaka 2023 na kumpisha mrithi wake lakini mkutano mkuu wa chama cha Cummunist uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana ulidhihirisha kuungwa mkono kukubwa kwa kiongozi huyo hali iliyopelekea kupandishwa hadhi na kuwa sawa na kiongozi muasisi wa taifa hilo, Mao Zedong.
Hata hivyo hatua ya bunge la China kupitisha pendekezo hilo haikuwa nyepesi kwani polisi walilazimika kukabiliana na wanaharakati vijana waliokuwa wanapinga hatua hiyo kufikiwa.
Wachambuzi wa siasa za China wamekuwa na mitazamo tofauti juu ya hatua hiyo huku wengine wakidai Jinping anapaswa kuachwa akamilishe kazi kubwa aliyoianza ya kuijenga nchi hiyo na kuisaidia kuwa miongoni mwa mataifa yenye uwezo na nguvu kubwa ya kiuchumi kwa sasa duaniani.
Lakini wachambuzi wengine wanadhani hatua hiyo ni ukandwamizwaji mkubwa wa demokrasia na uminywaji wa haki kwa raia wa China kuongozwa na viongozi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment