SEMA TU WANAUME NI WAVUMILIVU
Mademu kibao wametoa mimba zetu pasipo ridhaa zetu ila tumewasamehe na kumuachia Mungu yeye ndio mtoa hukumu.
Msichana mwengine Unamueleza vizuri kuwa una mke na una watoto, yeye ni mchepuko tu na kwamba hautaki mtoto wa nje ya NDOA lakini cha ajabu anakubebea mimba pasipo kukuambia tena anavunga Ikifika miezi Saba ndio anakwambia.
Wengine tulikuwa nao kwenye mahusiano as good time girls ila mwishowe kwa kufosi kuelewa wakaona solution ni kubeba mimba asa tungefanyaje, mtu hujampenda ama umeona huwezi kuishi nae as mkeo utamuoa kwa kuwa ana mimba yako?
Wengine ni mitego tu unakutana nae anamjua mkeo kabisa lakini anafokonyoa tu kwa kukubebea mimba ili aharibu NDOA yako ama anataka umuache mkeo umuoe yeye.
Msichana mwengine unamsomesha mpaka chuo kikuu, siku akipata degree yake anakuuliza ulitumia sh ngapi nikulipe? mbona tukifanyiwa hivi hatusemi tunajikaza kisabuni kiume tunakufa na maumivu yetu.
Wengine tumeoa ila tunalea watoto wa wengine humu humu ndani ya ndoa ila hatusemi tunaficha ibaki kuwa siri ya ndoa.
Wengine tunawaoa kwa kulazimishwa tu na bado tunaishi nao kwa roho kwetu..
Cha ajabu zaidi Licha Ya Changamoto zote wanaume wengi tunakubaligi kuwalea hao watoto tatizo lipo kwa Mama zao, Mtu anaishi nyumba ya kupanga kodi elfu 30 anataka umpe matumizi Ya mtoto laki 3 kwa mwezi, umdipositie 50 ktk junior account na umlipie bima Ya Afya mwaka mzima ilihali kipato chako anakijua, ndio maana tunaomua kama mbwae na iwe mbwae tu
Mheshimiwa Wanaume tuna malalamiko kibao hatuna pa kuyasemea...
(Jose Gizani)
#ModernTeacher
No comments:
Post a Comment