Meneja TRA Lindi matatani
Kamishna wa kodi za ndani TRA, Elijah Mwandubya amewasimamisha kazi watendaji wakuu wawili wa mamlaka hiyo mkoani Lindi kwa kile kilichodaiwa kuwa wamekiuka taratibu za utendaji kazi ndani ya mamlaka yake.
“Hatuwezi kuendelea kubaki na watu wachache ambao wanaharibu taswira ya serikali…hivyo basi tumekubaliana kwamba meneja wa malamlaka ya mapato mkoani Lindi John Msangi na afisa mkuu wa kodi mkoani humo Alfred Chembo wanasimamishwa kazi,”
Hatua za kusimamishwa kwa watendaji hao zimetokana na malalamiko ya wafanyabishara kutokuwa na ushirikiano baina yao na uongozi wa mamlaka ya mapato(TRA) mkoani Lindi hali inayochangiwa na ongezeko la kodi wanazokadiriwa.
Maamuzi hayo yamekuja siku mbili tu tangu wafanyabiashara hao walipotoa kilio chao mbele ya Azam TV katika mkutano wa wafanyabiashara mkoani Lindi.
Katika hatua nyingine, Mwandubya ameisimamisha kampuni ya Mchinga iliyokuwa ikitoa huduma ya uwakala wa kukusanya kodi za TRA mkoani Lindi na kuagiza wafanyabiashara wote walliofungiwa biashara zao kuendelea na biashara.
No comments:
Post a Comment